Friday, August 13, 2010

Harambee kigango cha Kiluvya


KANISA KATOLIKI KIGANGO CHA KILUVYA CHAFANYA HARAMBEE.
Tarehe 25 August, 2010, Kanisa Katoliki Kigango cha Kiluvya tumefanya Harambee kwa ajili ya kuanza Ujenzi wa Nyumba Ya Mapadre. Picha hiyo ni ya Kanisa letu la Kiluvya. ujenzi wake umekamilika. Limejengwa kwa Njia ya kujitegemea kupitia Waamini wenyewe. Katika Harambee Tajwa hapo juu Kanisa Katoliki Kiluvya tulipata bahati ya kumpata Balozi wa Msumbiji Nchini Tanzania kuwa Mgeni wetu rasmi. Naye ni Ndugu yetu Mheshimiwa Balozi Amour Zacharia Kupella ambae alifuatana na Mke wake.
Katika Harambee hiyo ambayo ni ya kwanza kwa ajili ya Ujenzi wa Nyumba ya Mapdre Mwenyezi Mungu alitubariki na tuliweza kupata Tshs. 42,902,000/= ( Milioni Arobaini na Mbili Laki Tisa na Mbili Elfu). Kati ya Pesa hizo Tumepata Pesa Taslim Tshs. 41,000,000/= na kiasi kidogo kilichosalia ni Ahadi ambazo tayari walioahidi wameanza kutoa. Hebu fuatili uone jinsi mambo yalivyokuwa hatua kwa hatua. Tafadhali usichoke. Mwisho tunakaribisha kwa yeyote mwenye Mapenzi mema ambaye ungependa kutuunga mkono kutuchangia tunawakaribisha sana.
Posted by Picasa

No comments:

Post a Comment

Weka Maoni Yako Hapa tafadhali,Wengi tunakubaliana na kauli ya kuwa mteja ni mfalme, katika Kiluvya tunasisitiza haki na heshima kwa wafanyakazi wetu pia, huku tukiamini nasi pia tunastahili kuangaliwa kwa kasi ile ile tunayoyowaangalia wateja wetu wote.karibuni sana.